Files
Download Full Text (42.2 MB)
Description
Dibaji
Mtaa huu wa Sukuma-Vuta kwa shule za mafunzo ya kilimo shambani (FFS) ni hatua kubwa katika kuingiza teknolojia ya Sukuma-Vuta katika mifumo ya utoaji ushauri kwa kilimo Afrika mashariki na kusini. Njia hii ya FFS inalenga kuwasaidia wakulima katika kuimarisha ubora wa teknolojia ya kusambaza na kuhakikisha wakulima wengi wanafaidika kutokana na teknolojia bunifu.
Ingawa taasisi za utafiti zimetayarisha teknolojia mrseto za kutatua matatizo ya uzalishaji katika mifumo mingi ya kilimo katika mashamba madogo, uzalishaji katika kilimo umeendelea kushuka. Teknolojia nyingi hazijasambazwa vyema kwa sehemu kubwa ya wakulima na hivyo kubaki kwa kiwango kidogo cha matumizi, isipokuwa katika sehemu ndogo ambapo zilifanyiwa majaribio. Itoshe, nyingine hazijajaribiwa katika mashamba ya wakulima ili kutoa fursa kwa mabadiliko kuambatana na hali za maeneo husika. Mbinu zisizofaa za usimamizi na kuendelea kuongezeka kwa mzigo katika rasilimali, hasa rasilimali asili na rasilimali za kiuchumi kumezidisha hali hii.
Mkakati wa Sukuma-Vuta ni teknolojia ya kimsingi iliyo na uwezo wa kuimarisha maisha ya familia za wakulima wa mashamba madogo na familia za mashambani, kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuimarisha uendelevu wa mazingira. Matokeo haya yanaweza kufikiwa kwa kuangazia matatizo ya kwekwe za striga, stemborer, na viwango vya chini vya rutuba kwenye mchanga. Haya ni matatizo makuu yanayohathiri uzalishaji na nafaka katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa jumla na hasa katika eneo la Afrika Mashariki. Utafiti uliofanywa na icipe, ikishirikiana na washirika wake, hasa KARI, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini Kenya, na Rothamsted Research nchini Uingereza, umeonyesha kuwa kupanda nyasi aina ya Napier (hasa aina ya Bana) kuzunguka shamba la mahindi lililopandwa mimea ya jamii ya maharagwe humo ndani, desmodium (silverleaf au greenleaf), hupunguza pakubwa matatizo ya striga na stemborer.
Teknolojia ya Sukuma-Vuta kwa sasa inatumiwa na wakulima zaidi ya 7000 katika wilaya 19 nchini Kenya, wilaya 5 Uganda, na mafunzo na maonyesho yameanza nchini Tanzania. Lengo letu ni kueneza teknolojia hii kwa wakulima wengi kadiri inavyowezekana katika maeneo tofauti ya kilimo-ikolojia, na majimbo. Ili kufanya hivyo, matumizi ya mfumo Shule za Mafunzo kwa Wakulima Shambani (FFS) yanafaa. Sukuma-Vuta ni teknolojia inayohitaji ujuzi mwingi na huhitaji mtaala uliotayarishwa vyema kuwawezesha wakulima kuelewa na kutumia katika mashamba yao. Mtaala ni mwongozo wa kutoa fursa nyingi za mafunzo katika njia nyingi kwa kuifikisha kwa wakulima wa mashamba madogo. Aidha, ni rasilimali muhimu katika mfumo wa kitaifa wa kutoa ushauri huduma na ushauri kwa wakulima, NGOs na mashirika ya kijamii.
icipe inatumaini kuwa mtaala huu utamairisha ufahamu wa wakulima wa mifumo ya kilimo na ikolojia, changamoto katika uzalishaji wa nafaka na uwezo wa teknolojia ya Sukuma-Vuta wa kuzitatua. Kadhalika, kuna matumaini kuwa itatia nguvu uwezo wa wakazi kufanya maamuzi na kustawisha teknolojia ili kuwawezesha kuwa na kilimo kinachozalisha zaidi na kilicho endelevu.
Prof. Christian Borgemeister
Mkurugenzi Mkuu, icipe, Nairobi, Kenya
ISBN
92 9064 229 7
Publication Date
2011
Publisher
International Centre of Insect Physiology and Ecology (icipe)
Recommended Citation
ICIPE. 2011. Mtaala wa Sukuma-Vuta kwa Mafunzo ya Wakulima Shambani. International Centre of Insect Physiology and Ecology, Nairobi, Kenya.